NACTE: PUBLIC INFORMATION ABOUT TECHINICAL EDUCATION AND TRAINING EXHIBITION. AT 31Th May 2019

NACTE

THE NATIONAL COUNCIL FOR TECHNICAL EDUCATION (NACTE)

 NACTE: PUBLIC INFORMATION ABOUT  TECHINICAL EDUCATION AND TRAINING EXHIBITION.  AT 31Th May 2019

Read more  in Swahili

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAONESHO YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI NCHINI
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), ni chombo kilichoanzishwa kwa mujibu wa Sheria, Sura ya 129. Kwa mujibu wa Sheria hiyo, Baraza linao wajibu wa kusimamia na kuhakikisha kuwa Elimu na Mafunzo ya Ufundi yanayotolewa nchini yanakidhi vigezo na ubora unaohitajika katika soko la ajira ndani na nje ya Tanzania.
Kwa sasa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais,  Dkt. John Joseph Pombe Magufuli imedhamiria kujenga nchi yenye uchumi wa Viwanda ifikapo mwaka 2025. Juhudi za kuifikisha nchi kwenye uchumi wa viwanda zimeshaanza kuonekana. Mikoa yote ilishaagizwa kuwa na viwanda na tayari viwanda vimeshajengwa na vinaendelea kujengwa.  Hivyo ni dhahiri kwamba, nguvu kazi ya kufanya kazi kwenye viwanda hivyo ambayo inazalishwa katika vyuo na taasisi za elimu ya ufundi inahitajika kwa kiasi kikubwa.

Katika muktadha huu, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi limeandaa maonesho ya kwanza ya elimu na mafunzo ya ufundi (Technical Education and Training Exhibitions) yatakayofanyika kuanzia tarehe 27 hadi 31 Mei, 2019 katika Uwanja wa Jamuhuri – Dododma. Maonesho hayo yatashirikisha Vyuo na Taasisi mbalimbali zinazotao Elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu ya ufundi.

Madhumuni ya maonesho hayo ni pamoja na: –
(i) Kutoa fursa kwa vyuo vyote, vinavyotao elimu na mafunzo ya ufundi kuonesha nini kinachofanyika kwenye vyuo vyao. Ni fursa adhimu kwao kujitangaza, kuwaelezea Watanzania nini wanachokifanya katika kuandaa wataalam katika sekta husika.
(ii) Kujenga ushirikiano madhubuti kati ya viwanda/waajiri na taasisi zinazotoa elimu na mafunzo ya ufundi.
(iii) Kutoa nafasi kwa wananchi kujionea na kujifunza nini kinafanyika kwenye vyuo vyetu vinavyoandaa wataalamu wenye ujuzi ambao wanahitajika sana kwenye soko la ajira, na hasa wakati huu tunapojenga uchumi wa viwanda. Hivyo udahili wa wanafunzi katika sekta ya elimu na mafunzo ya ufundi utaongezeka.
(iv) Kuwasaidia wananchi na hasa vijana katika kufanya maamuzi sahihi ya utaalam upi ajifunze  na wapi unapatikana.
(v) Kushirikishana uzoefu mbalimbali wa namna sayansi na teknolojia inavyotumika katika kutoa ubora wa elimu na mafunzo ya ufundi nchini.
(vi) Kutoa fursa ya kutangaza huduma mbalimbali zitolewazo na NACTE katika kuboresha elimu na mafunzo ya ufundi.

See also  NACTE: GUIDE BOOK 2019/2020

Hivyo, nitumie fursa hii kuhamasisha vyuo na taasisi mbalimbali zinazohusika na elimu na mafunzo ya ufundi nchini kushiriki katika maonesho. Vyuo, taasisi na wadau wengineo wa elimu na mafunzo ya ufundi wanatakiwa kudhibitisha ushiriki wao mapema kabla ya tarehe 31 Machi, 2019.

Kwa taarifa zaidi kuhusiana na maonesho haya, wasiliana na Baraza (NACTE) kupitia kwa Mr. Twaha A. Twaha kwa namba ya simu 0677019126 au  barua pepe: twaha@nacte.go.tz .

Imetolewa na Ofisi ya
Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
Tarehe: 18 Machi, 2019

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *